URUSI-MAREKANI-DIPLOMASIA

Kesi ya Navalny: Moscow yaahidi kuchukuwa hatua kwa vikwazo vya Washington

Sehemu ambapo mpinzani mkuu wa Kremlin Alexei Navalny anatumikia kifungo chake, huko Pokrov Februari 28, 2021.
Sehemu ambapo mpinzani mkuu wa Kremlin Alexei Navalny anatumikia kifungo chake, huko Pokrov Februari 28, 2021. REUTERS - Tatyana Makeyeva

Wakati Washington ilitangaza Jumanne Machi 2 vikwazo dhidi ya maafisa wakuu 7 wa Urusi, ikiwa ni pamoja na mkuu wa idara ya usalama, wakishtumiwa kuhusika katika jaribio la kumpa sumu Alexey Navalny, Urusi haikuchelewa kujibu.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka nchini Urusi inalaani uamuzi huo "wa kipuuzi na usio na maana yoyote "na imeahidi kujibu kuchukkuwa hatua dhidi ya vikwazo hivyo vya Marekani.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi Maria Zakharova alisema katika taarifa iliyotolewa Jumanne jioni Machi 2: "Tutachukua hatua kwa msingi wa ulipazaji kisasi. Itachukua siku kadhaa, hata hivyo, kujua hatua ambazo zitachukuliwa na Moscow.

Urusi inaedelea kushikilia msimamo wake: inakataa kutambua kuwa Alexei Navalny alipewa sumu na inalaani kuingiliwa kwa nchi za Magharibi kwa katika kile inachokiona kama masuala ya ndani. "Haya yote ni kisingizio" kwa "uchokozi wa kiuadui na dhidi ya Urusi," amesema Maria Zakharova.

Mamlaka ya Urusi imekuwa ikitarajia vikwazo hivi, na kwa uchaguzi wa Joe Biden pia ilitarajia kutakuepo na ugumu wa sera ya Marekai kwa Urusi. Walakini, matangazo yaliyotolewa na Washington yanabaki kulingana na kile kilichofanyika hapo awali na kama yale yaliyotolewa na Brussels pia katika mambo ya Navalny: hivi ni vikwazo vya kibinafsi, vinalenga idara za usalama na maafisa katika ofisi ya rais.