CHINA-HONG KONG-USALAMA-SIASA

Bunge la China lapendekeza "kuboresha" mfumo wa uchaguzi wa Hong Kong

China inaendelea na shinikizo kwa jimbo la Hong Kong>
China inaendelea na shinikizo kwa jimbo la Hong Kong> Xavier Tran Courtesy of Xavier Tran/AFP

Bunge la China limekuja na mapendekezo ya "kuboresha" mfumo wa uchaguzi huko Hong Kong, Shirika la habari la New China limeripoti Alhamisi wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii huenda ikabainisha uvumi mwingi juu ya mabadiliko makubwa yaliyoamuliwa na mamlaka nchini China kuhusu muundo wa kisiasa wa jiji hilo chini ya usimamizi maalum, ambapo tayari imefaulu kuweka sheria mpya ya usalama wa kitaifa kufuatia maandamano makubwa kuunga mkono demokrasia mnamo mwaka 2019.

China inatarajia kuweka wazi mpango mpya wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya kijamii na kiuchumi kwa mwaka 2021 katika kikao cha kila mwaka cha Bunge la nchi hiyo ambalo linalofunguliwa Ijumaa.