JAPANI-CHINA-AFYA

Covid: China yaombwa kusitisha vipimo vya sehemu ya haja kubwa kwa raia wa Japani

Mfanyakazi wa afya anachukua sampuli ya swab kutoka kwa mkazi katika mji wa Wuhan nchini China, ambayo wataalam wa WHO walitembelea katika kujaribu kugundua kiini cha virusi vya Covid-19.
Mfanyakazi wa afya anachukua sampuli ya swab kutoka kwa mkazi katika mji wa Wuhan nchini China, ambayo wataalam wa WHO walitembelea katika kujaribu kugundua kiini cha virusi vya Covid-19. Hector RETAMAL AFP

Japani imeitaka China kuacha kufanya vipimo vya ugonjwa wa Covid-19 kupitia sehemu ya haja kubwa kwa raia wake wanapoingia nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya raia wa Japani wamelalamika kwamba utaratibu huo umewasababishia "shida ya kisaikolojia", maafisa wamesema.

China, ambayo ina idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19i, ilianza kufanya vipimo vya sehemu ya haja kubwa mnamo mwezi Januari.

Wiki iliyopita, China ilikanusha madai ya wanadiplomasia wa Marekani kwamba mamlaka nchi humo iliwalazimisha kufanya vipimo kama hivyo baada ya vyombo vya habari vya Marekani kuripoti kwamba baadhi ya wanadiplomasia hao walilalamikia hali hiyo.