BURMA-MAREKANI-UNSC-DIPLOMASIA

Baraza la Usalama la UN kuijadili Burma

Raia wa Burma wanaoishi Thailand wakati wa maandamano nje ya jengo la Umoja wa Mataifa huko Bangkok mnamo Machi 4, 2021. Wanataka jumuiya ya kimataifa kuingilia kati baada ya mapinduzi ya Februari 1.
Raia wa Burma wanaoishi Thailand wakati wa maandamano nje ya jengo la Umoja wa Mataifa huko Bangkok mnamo Machi 4, 2021. Wanataka jumuiya ya kimataifa kuingilia kati baada ya mapinduzi ya Februari 1. AP - Sakchai Lalit

Wakati akizungumza kwa niaba ya Marekani juu ya Tigray Alhamisi wiki hii, baada ya Baraza la Usalama kutokubaliana juu ya taarifa ya pamoja, Balozi wa Marekani Linda Thomas-Greenfield amewashangaza wengi kwa kutangaza mkutano wa baraza hilo leo Ijumaa asubuhi  kuhusu Burma.

Matangazo ya kibiashara

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield Ametoa wito kwa wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuonyesha umoja na kuchukuwa maamuzio sahihi, wakati Umoja wa Mataifa ukijitahidi kufikia majenerali wa Burma wanaoshikilia madaraka, ambao wanaendelea kushambulia raia nchini humo.

Balozi Linda Thomas-Greenfield amesema hatua madhubuti zichukuliwe ili kuwalinda raia wa Burma wanaokandamizwa kwa kuwa wanatetea demokrasia.

Badala ya watawala wa kijeshi kuheshimu sheria na kujiepusha na vurugu na hatimaye kufuata njia ya mazungumzo, watawala hao wa wameongeza kasi ya kuwadhulumu watu wa Burma kwa miaka kadhaa sasa

.Kwa upande wake mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia suala la Burma, Thomas Andrews amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuweka vikwazo vya silaha na vya kiuchumi dhidi ya utawala wa kijeshi nchini Burma.

Thomas Andrews ameihimiza mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC kuchunguza na kisha kufungua mashtaka ya uhalifu na ukatili dhidi ya binadamu uliotokea nchini Burma.

Zaidi ya mwezi mmoja baada ya mapinduzi, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kukubaliana kutoa taarifa ya pamoja kuhusu Burma.