MYANMAR

Maandamano yaendelea Myanmar, wawili wauawa Myitkyina

Waandamanaji wakitawanywa kwa gesi ya kutoa machozi huko Yangoon Machi 8.
Waandamanaji wakitawanywa kwa gesi ya kutoa machozi huko Yangoon Machi 8. REUTERS - STRINGER

Waandamanaji wawili wameuawa nchini Myanmar leo Jumatatu, baada ya kupigwa wrisasi kichwani kulingana na mashuhuda, wakati viwanda, benki na biashara zimefungwa huko Yangon, jiji kubwa zaidi nchini.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo imekuja kufuatia wito wa chama cha wafanyakazi wa kutaka kuzorotesha uchumi kama sehemu ya maandamano dhidi ya mapinduzi ya kijeshi ya Februari 1.

Kwenye mtandao wa Facebook, picha zinaonyesha miili ya watu wawili ikiwa imelazwa barabarani huko Myitkyina, kaskazini mwa nchi. Mashuhuda wanasema w hao wawahanga hao wawili walikuwa wakishiriki katika maandamano wakati maafisa wa polisi walir na mabusha gruneti na mabomu ya machozi. Watu kadhaa wakati huo wa,ejeruhiwa kwa risasi kutoka majengo yaliyo karibu.

Shahidi wa miaka 20 ameliiambia shirika la habari la Reuters kuwa watu wawili wamepigwa risasi kichwani na kufa papo hapo. Watu wengine watatu wamejeruhiwa.

"Ni unyama kuua raia wasio na silaha," ameshutumu shahidi huyu. "Tunapaswa kuwa na haki ya kuandamana kwa amani."

Haijafahamika mara moja wahusika wa kitendo hiki. Polisi na wanajeshi wametumwa katika maeneo mbalimbali kuzima maandamano hayo, mashahidi wanasema.

Vikosi vya Myanmar vimewauwa zaidi ya watu 50 tangu mapinduzi ya Februari 1, kulingana na ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa wiki iliyopita.