MYANMAR

Myanmar: Hali ya taharuki yatanda Yangon, raia watoroka makaazi yao

Mtu aliyepigwa risasi na vikosi wa usalama dhidi ya waandamanaji wanaopinga mapinduzi huko Thingangyun, Yangon.
Mtu aliyepigwa risasi na vikosi wa usalama dhidi ya waandamanaji wanaopinga mapinduzi huko Thingangyun, Yangon. REUTERS - Stringer .

Wakazi wa mji wa Yangon wameendelea kuyatoroka makaazi yao kwa wingi leo Jumanne. Mji wa Yangon ulikumbwa na mapigano makali katika siku za hivi karibuni, wakati ambapo familia za waandamanaji wanaotetea demokrasia wakijiandaa kuzika wapendwa wao waliouawa na vikosi vya usalama.

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya watu 180 wameuawa tangu mapinduzi ya Februari 1 dhidi ya Aung San Suu Kyi, kulingana na Chama cha kinachotoa huduma kwa Wafungwa wa Kisiasa (AAPP).

Idadi ya vifo imeongezeka katika siku tatu zilizopita, huku viongozi wa mapinduzi wakichukuwa hatua kali zaidi kwa kuwakandamiza waandamanaji kuliko hapo awali na kupuuzia mbali shutma kutoka nchi mbalimbali duniani.

Angalau waandamanaji 20 waliuawa siku moja kabla, kulingana na AAPP. Jumapili watu 74 waliuawa kwa kupigwa risasi, viongozi wa mapinduzi wakibaini kwamba walipoteza afisa wa polisi.