MAREKANI-URUSI

Biden: Putin atakiona cha mtima kuni kwa kuingilia uchaguzi wa Marekani

Joe Biden atoa onyo la kutahadharisha Urusi kuhusu juhudi zake za kuingilia uchaguzi wa Marekani.
Joe Biden atoa onyo la kutahadharisha Urusi kuhusu juhudi zake za kuingilia uchaguzi wa Marekani. REUTERS - KEVIN LAMARQUE

Rais wa Marekani Joe Biden amesema Vladimir Putin atajuta kwa juhudi zake za kujaribu kushawishi uchaguzi wa urais wa mwaka wa 2020 nchini Marekani kwa niaba ya Donald Trump.

Matangazo ya kibiashara

"Atakiona cha mtima kuni," rais wa Marekani amesema kuhusiana na mwenzake wa Urusi katika mahojiano yaliyorushwa Jumatano na kituo cha ABC News.

Alipoulizwa juu ya aina ya athari atakayoipata Vladimir Putin, Joe Biden amejibu: "Utaiona hivi karibuni."

Ripoti ya ujasusi ya Marekani iliyotolewa Jumanne wiki hii inaunga mkono shutuma za muda mrefu kwamba baadhi ya maafisa wa jeshi wa Donald Trump walishirikiana na Urusi kwa kuongeza mashtaka kutoka maafisa Ukraine wenye uhusiano wa karibu na Moscow dhidi ya mpinzani wa wakati huo Joe Biden kutoka chama cha Democratic, kabla ya uchaguzi wa mwezi Novemba 2020.

Urusi kwa upande wake imesema madai hayo hayana msingi wowote.