KOREA KASKAZINI

Korea Kaskazini kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Malaysia

Bendera ya Korea Kaskazini kwenye ubalozi wa Korea Kaskazini huko Kuala Lumpur, Malaysia Machi 9, 2017.
Bendera ya Korea Kaskazini kwenye ubalozi wa Korea Kaskazini huko Kuala Lumpur, Malaysia Machi 9, 2017. REUTERS - Edgar Su

Korea Kaskazini imesema itavunja uhusiano wa kidiplomasia na Malaysia baada ya mahakama ya Malaysia kuidhinisha kupelekwa kwa raia wa Korea Kaskazini kwenda nchini Marekani ili kushtakiwa kwa utakatishaji wa fedha haramu, shirika la habari la serikali ya Pyongyang imeripoti.

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya nje ya Korea Kaskazini pia imeonya kuwa Marekani "itakiona cha mtima kuni", kulingana na taarifa iliyorushwa na shirika la habari la KCNA.

Mapema mwezi huu, Mahakama ya juu nchini Malaysia ilitoa uamuzi kwamba Mun Chol-myong anaweza kupelekwa nchini Marekani kushtakiwa, kulingana na ripoti za vyombo vya habari nchini Korea Kaskawini.

Mun alikamatwa mnamo mwaka 2019 baada ya mahakama ya Marekani kumshtaki kwa utakatishaji wa fedha na ulaghai uliolenga kusaidia usafirishaji haramu kwenda Korea Kaskazini. Analaani ombi la ku nchini Marekani kwa sababu za kisiasa.