China: Mtu mmoja ajilipua na kuua wanne
Imechapishwa:
Mtu mmoja amejiua na vilipuzi Jumatatu katika kitongoji cha kusini mwa China cha Canton, na pia kuua watu wengine wanne, polisi imesema.
Mlipuko huo ulitokea katika jengo moja katika mji wa Mingjing saa 10:00 asubuhi, saa za China na pia kuwajeruhi watu wengine watano , polisi imesema kwenye mtambo wa ujumbe wa Weibo.
"Majeruhi wote wamepelekwa katika hospitali kwa matibabu na uchunguzi zaidi unaendelea kuhusu ktkio hilo" polisi iimeongeza, na kubaini kwamba, kulingana na ripoti ya awali ya uchunguzi, mhusika wa mlipuko huo alikuwa mkazi wa miaka 59 aliyejulikana kwa jina la Hu.
Halmashauri ya manispaa ya eneo hilo inafanyia kazi katika jengo ambalo mlipuko huo ulitokea.