BURMA-EU

EU kuwachukulia vikwazo maafisa11 waliohusika mapinduzi Burma

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell,
Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell, REUTERS - JOHANNA GERON

Umoja wa Ulaya (EU) imesema itawachukulia vikwazo dhidi ya watu 11 waliohusika katika mapinduzi ya serikali chii Burma mapema mwezi Feruari, Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell ametangaza leo Jumatatu kabla ya mkutano wa mawaziri wa biashara kutoka umoja huo,

Matangazo ya kibiashara

Wakati Umoja wa Ulaya uliweka vikwazo vya silaha kwa nchi ya Burma na unalenga maafisa wengine wakuu wa jeshi tangu 2018, hatua hizi ni muhimu kwa EU kwa utawala wa kijeshi tangu mapinduzi.

"Tutachukua vikwazo dhidi ya watu 11 waliohusika katika mapinduzi na ukandamizaji dhidi ya waandamanaji," amesema Mwakilishi Mkuu wa umoja wa Ulaya wa Sera za nje na Sera za Usalama.

Majina ya watu hao yanatarajiwa kuwekwa hadharani mara tu vikwazo vikiamuliwa rasmi na mawaziri.

Hatua kali zaidi zinatarajiwa hivi karibuni, haswa dhidi ya kampuni zinazosimamiwa na jeshi.

Wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya waliliambia shiorika la habari la REUTERS kwamba makampui mawili yanayomilikiwa na jeshi, Myanmar Economic Holdings Limited (MEHL) na Shirika la Uchumi la Myanmar (MEC), huenda yakilengwa.