BANGLADESHI

400 watoweka baada ya moto kuzuka katika kambi ya wakimbizi ya Rohingya

Kambi ya wakimbizi ya Rohingya baada ya moto kuzuka katika baadhi ya nyumba huko Cox's Bazar, Bangladesh, Machi 23, 2021..
Kambi ya wakimbizi ya Rohingya baada ya moto kuzuka katika baadhi ya nyumba huko Cox's Bazar, Bangladesh, Machi 23, 2021.. REUTERS - STRINGER

Wakimbizi 400 wa Rohingya wametoweka baada ya moto mkubwa kuzuka katika kambi ya wakimbizi kusini mashariki mwa Bangladesh.

Matangazo ya kibiashara

Tukio nilo lilitokea siku ya Jumatatu na lilidumu saa kumi, likisababisha papo hapo vifo vya watu 15 na wengine 600 kujeruhiwa, kulingana na ripoti ya awali kutoka Umoja wa Mataifa na mamlaka nchini humo. Watu 45,000 watahamishwa kutoka makazi yao.

Karibu watu milioni moja kutoka jamii ya Rohingya , Waislamu walio wachache nchini Burma, wanaishi katika mazingira magumu nchini Bangladesh katika nyumba zilizotengenezwa na mianzi na maturubai katika kambi za wilaya ya Cox's Bazar, baada ya kukimbia mateso ya kijeshi nchini mwao mnamo mwaka 2017.

Nyumba 10,000 zateketea kwa moto

Moto wa siku ya Jumatatu ambao uliwaka kwa karibu saa kumi uliharibu nyumba karibu 10,000, kulingana na Mohsin Chowdhury, katibu wa idara ya usimamizi wa majanga na misaada, akibainisha kuwa kamati imeundwa ili kuchunguza tukio nilo. Angalau watu 15 wamepoteza maifa, 400 hawajulikani waliko na makumi ya maelfu wanapaswa kuhamishwa.

Wakimbizi hao "watahamishiwa katika nyumba zingine katika kambi hiyo," amesema Johannes van der Klaauw, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini Bangladesh, na kuongeza kuwa shirika hilo llina nafasi kwenye kambi hiyo na " hakuna ulazima wa kuwahamisha nje ya eneo la kambi ”.

Dola milioni 20 zahitajika kukidhi mahitaji ya haraka

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM laahidi msaada wa dola milioni 1 kwa haraka, na llimeonya kuwa dola milioni 20 zitahitajika kukidhi mahitaji ya haraka.