CHINA

Uyghurs: EU, Canada na Marekani waichukulia vikwazo China, Beijing yajibu

Nchi thelathini na tisa ziliitaka China, katika tamko la pamoja, kuheshimu haki za binadamu za watu kutoka jamii ya Uyghur huko Xinjiang.
Nchi thelathini na tisa ziliitaka China, katika tamko la pamoja, kuheshimu haki za binadamu za watu kutoka jamii ya Uyghur huko Xinjiang. REUTERS/Mike Segar

Umoja wa Ulaya, Marekani na Canada wameidhinisha tangu Jumatatu wiki hii vikwazo dhifi ya China kutokana na kuwafanyia udhalimu Waislamu kutoka jamii ya walio wachache ya Uyghur katika mkoa wa Xinjiang, na Beijing haikusita kulipiza kisasi kwa kuchukuwa vikwazo dhidi ya maafisa kadhaa wa umoja huo.

Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wameidhinisha vikwazo dhidi ya viongozi wanne na kampuni mmoja kutoka mkoa wa China wa Xinjiang.

Uingereza na Canada wamechukua hatua sawa na Umoja wa Ulaya. Vikwazo vya Umoja wa Ulaya na Uingereza dhidi ya ukiukaji wa haki za binadamu uliyotekelezwa na Beijing ni vya kwanza tangu mwaka 1989.

Marekani imeidhinisha vikwazo dhidi ya maafisa wawili wa China kati ya wanne waliowekewa vikwazo na Umoja wa Ulaya . Vikwazo vya Umoja wa Ulaya ni pamoja na marufuku ya kusafiri kwenda katika nchi yoyote mwanachama wa umoja huo na kuzuia mali zao zilizoshikiliwa katika Umoja wa Ulaya. Vikwazo vya Marekani "vinajazia" vile za Umoja wa Ulaya na Canada, kulingana na Washington.

China yalipiza kisasi

Beijing imejibu uamuzi wa Umoja wa Ulaya kwa kuiwachukulia vikwazo maafisa kumi  wa umoja huo, ikiwa ni pamoja na wabunge kadhaa waliochaguliwa katika Bunge la Ulaya, waliotuhumiwa "kwa kudhoofisha uhuru na masilahi ya China na kueneza uwongo na habari mbaya". Mashirika manne ya Umoja wa Ulaya pia yanahusika, ikiwa ni pamoja na Alliance of Democracies, taasisi ya Denmark iliyoongozwa na Katibu Mkuu wa zamani wa Jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi (NATO) Anders Fogh Rasmussen. Viongozi wa UUmoja wa Ulaya na familia zao watapigwa marufuku kuishi China.