CHINA

Coronavirus: Visa vipya 10 vya maambukizi vyathibitishwa China

Wahudumu wa afya wakisimama nje ya ofisi zao wakati wa kikao kilichoandaliwa na serikali kwa minajili ya wageni kupokea chanjo dhidi ya janga la COVID-19, katika kituo cha kutoa chanjo huko Beijing, China Machi 23, 2021.Wahudumu wa afya wakisimama nje ya ofisi zao wakati wa kikao kilichoandaliwa na serikali kwa minajili ya wageni kupokea chanjo dhidi ya janga la COVID-19, katika kituo cha kutoa chanjo huko Beijing, China Machi 23, 2021.
Wahudumu wa afya wakisimama nje ya ofisi zao wakati wa kikao kilichoandaliwa na serikali kwa minajili ya wageni kupokea chanjo dhidi ya janga la COVID-19, katika kituo cha kutoa chanjo huko Beijing, China Machi 23, 2021.Wahudumu wa afya wakisimama nje ya ofisi zao wakati wa kikao kilichoandaliwa na serikali kwa minajili ya wageni kupokea chanjo dhidi ya janga la COVID-19, katika kituo cha kutoa chanjo huko Beijing, China Machi 23, 2021. REUTERS - CARLOS GARCIA RAWLINS

China imerekodi visa vipya 10 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corina kwa siku moja, kutoka visa 9 siku moja iliyopita, maafisa wa afya wamesema.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa, Tume ya kitaifa ya Afya imesema watu waliopatiana na maambukizi hayo waliwasili nchini humo wakitokea nchi za kigeni.

Kulingana na takwimu rasmi, visa 90,125  vya maambukizi vimerekodiwa katika China Bara.

Idadi ya visa vya maambukizi inaendelea kuongezeka nchini humo, huku idadi ya vifo ikifikia 4,636.