Marekani na EU wakubaliana kushirikiana kuhusu China na Urusi
Imechapishwa:
Marekani na Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuzindua mazungumzo ya pande mbili kuhusu China na kufanya kazi pamoja kujibu "tabia mbaya" ya Urusi, kulingana na taarifa iliyotolewa kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken naa mkuu wa wa sera za mambo ya nje wa Ulaya, Josep Borrell Jumatano wiki hii.
Washington na Brussels zimekiri kugawana maono kwamba uhusiano na Beijing ulikuwa "na mambo mengi, na masuala ya ushirikiano, ushindani na uhasama wa kimfumo," imesema taarifa hiyo.
Kwenye hotuba hiyo, Blinken alijizuia kutoa maneno makali ya kuikosoa China na badala yake alitoa mwito kwa washirika wake kuungana na Marekani.
Blinken, alirudia msimamo wa Marekani wa kuiunga mkono NATO, akisema nchi hiyo imejitolea kikamilifu, ikiwa ni pamoja na kutekeleza kifungu cha 5, kinachoelezea wajibu wa kuhakikisha ulinzi miongoni mwa wanachama.
Wakati wa mkutano wao huko Brussels, Antony Blinken na Josep Borrell walijadili ushirikiano katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa, chanjo dhidi ya virusi vya Corona, Iran na Uturuki.