KOREA KASKAZINI

Korea Kaskazini yaituhumu UN kwa unduma kuwili kwa urushaji makombora

Siku ya Alhamisi Pyongyang ilisema  ilizindua aina mpya ya kombora la masafa mafupi, na kusababisha Washington kuomba mkutano wa kamati ya vikwazo ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini.
Siku ya Alhamisi Pyongyang ilisema ilizindua aina mpya ya kombora la masafa mafupi, na kusababisha Washington kuomba mkutano wa kamati ya vikwazo ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini. Jung Yeon-je / AFP

Korea Kaskazini imetangaza leo Jumatatu kwamba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikuwa likitumia kauli mbili tofauti, baada ya kamati ya Umoja wa Mataifa kulaani majaribio ya makombora yaliyofanywa hivi karibuni na Pyongyang kama ukiukaji wa maazimio ya Umoja wa Mataifa.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Alhamisi Pyongyang ilisema  ilizindua aina mpya ya kombora la masafa mafupi, na kusababisha Washington kuomba mkutano wa kamati ya vikwazo ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini.

Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya nje ya Korea Kaskazini ameripoti kwamba wakati wa mkutano huo, Marekani ilitaka Korea Kaskazini iongezewe vikwazo na kuimarisha utekelezaji wa hatua zilizopo dhidi yake.

Katika taarifa iliyorushwa na shirika la habari la serikali, KCNA, Jo Chol-su amesema mkutano huo "ulikusudia kunyima haki ya nchi yetu ya kujilinda", akionya kuwa "hatua ya kupinga" uwezekano wowote inaandaliwa.