URUSI

Urusi: Navalny kutenganishwa na wafungwa wengine

alilalamika katika siku za hivi karibuni kuwa anateswa kwa kunyimwa usingizi na aliomba kuweza kutembelewa na daktari wa kiraia kwa sababu ya maumivu makali anayoyapata mgongoni na mguuni, ombi lililokataliwa na mamlaka ya magereza..
alilalamika katika siku za hivi karibuni kuwa anateswa kwa kunyimwa usingizi na aliomba kuweza kutembelewa na daktari wa kiraia kwa sababu ya maumivu makali anayoyapata mgongoni na mguuni, ombi lililokataliwa na mamlaka ya magereza.. REUTERS - Shamil Zhumatov

Mwanasiasa wa upinzani nchini Urusi Alexeï Navalny ametangaza leo Jumatatu kwamba anaweza kutenganishwa na wafungwa wenzake kufuatia makosa madogo kadhaa yanayodaiwa dhidi yake na mamlaka ya magereza.

Matangazo ya kibiashara

Mpinzani wa Urusi Alexeï Navalny ametangaza Jumatatu kwamba anaweza anaweza kutenganishwa na wafungwa kufuatia makosa madogo kadhaa yanayodaiwa dhidi yake na mamlaka ya mgereza.

Mpinzani mkuu wa Vladimir Putin, aliyehukumiwa mapema mwezi Februari kifuungo cha miaka miwili na miezi minane katika kesi iliyoanza mwaka 2014, alitumwa mwishoni mwa mwezi uliopita kuzuiliwa katika IK-2, kwenye umbali wa kilomita 100, mashariki mwa mji wa Moscow.

Kwenye akaunti yake ya Instagram, Alexeï Navalny anasema alipokea karipio sita katika kipindi cha wiki mbili, akimaanisha kuwa maonyo mawili yanatosha kuhalalisha kuwekwa kwenye sehemu ya peke yake yake kwa kuendelea kutumikia kifungo chake. Kesi yake inatarajiwa kuchunguzwea na mahakama ya ndani ya jela, ameongeza.

Akiwa na umri wa miaka 44, mpinzani wa Vladimir Putin alilalamika katika siku za hivi karibuni kuwa anateswa kwa kunyimwa usingizi na aliomba kuweza kutembelewa na daktari wa kiraia kwa sababu ya maumivu makali anayoyapata mgongoni na mguuni, ombi lililokataliwa na mamlaka ya magereza.