BRAZILI

Coronavirus: Zaidi ya kesi mpya 100,000 za kila siku zaripotiwa nchini India

Pamoja na visa 103,558 vilivyoripotiwa Jumatatu, idadi ya visa vya maambukizi nchini India imeongezeka hadi visa  milioni 12.6,
Pamoja na visa 103,558 vilivyoripotiwa Jumatatu, idadi ya visa vya maambukizi nchini India imeongezeka hadi visa milioni 12.6, REUTERS - FRANCIS MASCARENHAS

India imerekodi idadi kubwa ya visa vya maambukizi ya kila siku ya virusi ya Corona, na zaidi ya maambukizi 100,000 yametangazwa na Wizara ya Afya Jumatatu wiki hii, ikiwa ni mara ya kwanza nci hi kuvuka kizingiti tangu kuzuka kwa mgogoro wa kiafya.

Matangazo ya kibiashara

Mbali na Marekani, hakuna nchi yoyote ulimwenguni ambayo imerekodi zaidi ya kesi mpya 100,000 kwa siku moja.

Pamoja na visa 103,558 vilivyoripotiwa Jumatatu, idadi ya visa vya maambukizi nchini India imeongezeka hadi visa  milioni 12.6, ikiwa ni nchi ya tatu yenye wagonjwa wengi zaidi ulimwenguni baada ya Marekani na Brazil, na kufikisha idadi ya vifo hadi 165,101, na vifo vya kila 478 vimeripotiwa kwa siku moja.