AUSTRIA

Iran na Marekani zaanza mazungumzo kuhusu nyuklia

Aprili 6, pande husika kwenye mkataba wa mpango wa nyuklia wa Iran, Urusi, China, nchi za Ulaya na Iran wamekusanyika kujadili kuondolewa kwa vikwazo vya Marekni na Iran kurudi kuheshimu ahadi zake
Aprili 6, pande husika kwenye mkataba wa mpango wa nyuklia wa Iran, Urusi, China, nchi za Ulaya na Iran wamekusanyika kujadili kuondolewa kwa vikwazo vya Marekni na Iran kurudi kuheshimu ahadi zake via REUTERS - EU Delegation in Vienna

Iran na Marekani zimeanza mazungumzo ya moja kwa moja huko Vienna Jumanne kwa lengo la kurudisha nchi hizo mbili chini ya mkataba wa mpango wa nyuklia wa Tehran wa mwaka 2015, mchakato ambao Washington ilivunja miaka mitatu iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Kujiondoa kwa Marekani kwenye mkataba huo kulisababisha Tehran kuvuka mara kwa mara mipaka iliyowekwa na mkataba kwa shughuli zake za kuimarisha Uranium, na kusababisha kurudi kwa vikwazo ambavyo vinasumbua uchumi wa jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Jumatatu wiki hii Washington ilisema inatarajia mazungumzo hayo mapya yatakuwa magumu na hakuna upande unaotarajia maendeleo makubwa.

"Bado hatuna matumaini juu ya matokeo ya mkutano huu, lakini tuna uhakika kwamba tuko kwenye njia sahihi na ikiwa Marekani itaonyesha nia njema, umakini na uaminifu, hiyo inaweza kuwa ishara nzuri kwa mustakabali mzuri wa mkataba huu na zaidi kwa utekelezaji wake kamili, "msemaji wa serikali ya Iran Ali Rabiei aliwaambia waandishi wa habari.

Wawakilishi wa Uingereza, Ufaransa na Ujerumani watatumika kama wasuluhishi kati ya Marekani na Iran katika mji mkuu wa Austria, ambapo mkataba wa mwaka 2015 yalikamilishwa. Wajumbe kutoka China na Urus pia watakuwepo.