URUSI

Urusi: Vladimir Putin ajiruhusu kualia madarakani hadi mwaka 2036

Rais wa Urusi Vladimir Putin huko Moscow, Machi 31, 2021.
Rais wa Urusi Vladimir Putin huko Moscow, Machi 31, 2021. AP - Alexei Druzhinin

Rais wa Urusi Vladimir Putin, 68, alisaini sheria hiyo Jumatatu, Aprili 5, ikimruhusu kuwania mihula mipya miwili katika kusalia kwenye kiti cha urais.

Matangazo ya kibiashara

Mwezi Desemba 2020 rais wa Vladmir Putin alisaini sheria inayotoa kinga ya kutoshitakiwa kwa waliokuwa marais wa nchi hiyo.

Sheria hiyo vile vile inatoa fursa kwa marais wa zamani kuwa maseneta wa maisha katika bunge la juu la nchi hiyo, punde tu wanapoondoka madarakani.

Sheria hiyo inafuatia mabadiliko makubwa ya kisiasa ambayo yalifanywa na Putin nchini Urusi, mwaka wa 2020.

Sheria hiyo ni sehemu ya mabadiliko ya katiba yaliyopitishwa kote nchini humo mwaka jana, na kumruhusu Putin kusalia madarakani hadi mwaka 2036.

Alikuwa anatarajiwa kuondoka madarakani mwaka 2024.