URUSI

Amnesty: Yasadikiwa kuwa Urusi inamuangamiza polepole Navalny

Alexei Navalny wiki iliyopita alianza mgomo wa njaa kwa matumaini ya kutaka mamlaka ya gereza ambalo anazuiliwa karibu na mji mkuu wa Moscow kumpatia matibabu sahihi ambayo anaomba, akitaja maumivu makali ya mgongo na mguu.
Alexei Navalny wiki iliyopita alianza mgomo wa njaa kwa matumaini ya kutaka mamlaka ya gereza ambalo anazuiliwa karibu na mji mkuu wa Moscow kumpatia matibabu sahihi ambayo anaomba, akitaja maumivu makali ya mgongo na mguu. REUTERS - MAXIM SHEMETOV

Mwanasiasa wa upinzani ncini Urusi Alexei Navalny anashikiliwa katika mazingira ambayo ni sawa na kuteswa na inaweza kusababisha kifo chake polepole, limesema shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International, ambalo linachapisha ripoti yake ya kila mwaka leo Jumatano.

Matangazo ya kibiashara

Amnesty International inasema imesikitishwa na kuona mkosoaji mkuu wa Kremlin ananyimwa haki ya kuonana na daktari anayemtaka gerezani huku akifanyiwa madhila mbalimbali.

"Urusi, mamlaka ya Urusi, inawezekana kuwa walimuweka katika mazingira mabaya ya kumsababishia kifo na kutafuta kuficha kile kinachomsibu," katibu mkuu wa Amnesty International Agnes Callamard ameliambia shirika la habari la REUTERS kabla ya kuchapishwa kwa Ripoti ya Mwaka.

"Ni wazi mamlaka ya Urusi inakiuka haki zake. Tunahitaji kupambana vilivyo," ameongeza. "Wamejaribu kumuua, sasa wanamzuia, na wakiweka masharti magumu ya kuzuia jela ambayo ni sawa na kuteswa."

Alexei Navalny wiki iliyopita alianza mgomo wa njaa kwa matumaini ya kutakamamlaka ya gereza ambalo anazuiliwa karibu na mji mkuu wa Moscow kumpatia matibabu sahihi ambayo anaomba, akitaja maumivu makali ya mgongo na mguu.