KOREA KUSINI

Coronavirus: Korea Kusini yakabiliwa na ongezeko la visa vipya

Korea Kusini inashuhudia mlipuko wa pili wa janga la Corona.
Korea Kusini inashuhudia mlipuko wa pili wa janga la Corona. Jung Yeon-je / AFP

Korea Kusini imerekodi visa vipya 668 vya maambukizi ya virusi vya Corona kwa siku moja, kulingana na takwimu rasmi zilizotolewa Jumatano, ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya kila siku tangu Januari 8 katika kuongezeka kwa mlipuko mpya wa maambukizi.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na data kutoka kwa mamlaka ya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (KDCA), jumla ya visa vya maambukizi vimefikia 106,898, wakati vifo 1,756 vimeripotiwa nchini humo tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Korea Kusini.

Zaidi ya 63% ya kesi mpya zimerekodiwa katika mji mkuu wa Seoul na maeneo jirani, takwimu kutoka KDCA zinaonyesha.