Coronavirus: Zaidi ya kesi mpya 115,000 zathibitishwa nchini India
Imechapishwa:
India imerekodi visa vipya 115,736 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona kwa siku moja, kulingana na takwimu rasmi zilizotolewa leo Jumatano, ikiwa ni rekodi ya kila siku tangu kuzuka kwa mgogoro wa kiafya nchini humo.
Takwimu kutoka Wizara ya Afya pia zinaripoti vifo vipya 630 kutokana na COVID-19, na kusababisha idadi ya vifo kufikia 166,177.
Virusi vya Corona (Cov) ni familia ya virusi vinavyosababisha ugonjwa kuanzia mafua ya kawaida hadi magonjwa makali zaidi kama vile matatizo ya kupumua (MERS-CoV) na SARS-CoV.
Virusi vya Corona vya COVID-19 ni mripuko mpya uliogunduliwa mwaka 2019 na havikuwahi kubainika hapo kabla miongoni mwa bindamu. Dalili zake ni pamoja na homa, kikohozi, shida katika kupumua, na katika hali ngumu zaidi, maambukizi yanaweza kusababisha, nimonia, kukosa pumzi, kushindwa kufanyakazi kwa figo na hata kifo.