IRAN

Iran yadai kushambuliwa kwa moja ya meli zake katika Bahari Nyekundu

Meli ya Iran, Saviz, kulingana na serikali ni meli ya kibiashara, chombo cha kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi kulingana na vyanzo vingine, hapa ilipigwa picha mwezi Oktoba 2020. Chombo hicho kililipuka katika Bahari ya Shamu Aprili 6.
Meli ya Iran, Saviz, kulingana na serikali ni meli ya kibiashara, chombo cha kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi kulingana na vyanzo vingine, hapa ilipigwa picha mwezi Oktoba 2020. Chombo hicho kililipuka katika Bahari ya Shamu Aprili 6. AP - Planet Labs Inc.

Meli ya Irani, Saviz, imeshambuliwa katika Bahari Nyekundu, wizara ya mambo ya nje ya Iran imesema leo Jumatano, wakati vyombo vya habari vimeripoti kuwa meli hiyo imeshambuliwa kwa kutumia mabomu aina ya Limpet yanayotegwa katika meli.

Matangazo ya kibiashara

"Mlipuko huo ulitokea Jumanne asubuhi karibu na pwani ya Djibouti na kusababisha uharibifu mdogo bila kusababisha majeruhi yoyote.

Meli hiyo ni ya kiraia inayopiga doria katika bahari hiyo ili kuhakikisha usalama wa eneo unalindwa dhidi ya maharamia," msemaji wa wizara hiyo Saeed Khatibzadeh amesema, na kuongeza kuwa uchunguzi umeanzishwa.

Mashambulio kadhaa kwa meli za kibiashara za Israeli na Iran yameripotiwa katika eneo hilo tangu mwezi Februari, na kila nchi ikimtuhumu mwenzake kuhusika.