CHINA

China yaionya Marekani kuhusu Taiwan

Zhao Lijian, msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China, amewaambia waandishi wa habari kuwa "taarifa kali" zimewasilishwa kwa Marekani.
Zhao Lijian, msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China, amewaambia waandishi wa habari kuwa "taarifa kali" zimewasilishwa kwa Marekani. REUTERS - TYRONE SIU

China imeionya Marekani "isicheze na moto" kuhusu Taiwan baada ya Washington kutoa mwongozo mpya wa kuwezesha mawasiliano kati ya maafisa wa Marekani na Taiwan

Matangazo ya kibiashara

Mpango uliotangazwa na wizara ya mambo ya nje ya Marekani kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na Taiwan unakuja wakati kukiendelea operesheni za jeshi la China karibu na kisiwa hicho, ambacho inakichukulia kama mkoa wa waasi ambao unatakiwa kudhibitiwa kwa nguvu ikiwa ni lazima. Ndege za kivita za China zinafanya mazoezi ya kijeshi, huku zikionekana kila siku katika anga ya Taiwan.

Zhao Lijian, msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China, amewaambia waandishi wa habari kuwa "taarifa kali" zimewasilishwa kwa Marekani.

China imeionya Maekani "kutocheza na moto juu ya suala la Taiwan, na imetakiwa kusitisha mara moja aina zote za mazungumzo rasmi kati ya Marekani na Taiwan, kushughulikia jambo hili kwa uangalifu na ipasavyo, na sio kupeleka ishara mbaya kwa vikosi vinavyopigania uhuru  huko Taiwan ili tusivuruge uhusiano kati ya China na Marekani na amani na utulivu kote kwenye Mlango wa Taiwan, "amesema.