MAREKANI

John Kerry njiani kuelekea China na Korea Kusini

Mjumbe Maalum wa rais wa Marekani anayehusika na masuala ya Tabianchi, John Kerry, atakuwa afisa wa kwanza kutoka kwa utawala wa rais Joe Biden kuzuru China.
Mjumbe Maalum wa rais wa Marekani anayehusika na masuala ya Tabianchi, John Kerry, atakuwa afisa wa kwanza kutoka kwa utawala wa rais Joe Biden kuzuru China. Ludovic MARIN AFP/File

Mjumbe wa Marekani anayehusika na masuala ya Tabianchi, John Kerry, anasafiri kwenda China wiki hii kujadili juhudi za kimataifa za kupambana na ongezeko la joto duniani, kwa lengo la kuwashawishi wenzake kuweka malengo zaidi ya kupunguza uzalishaji wa gesi chafu, licha ya mivutano kati ya China na Marekani.

Matangazo ya kibiashara

John Kerry anatarajiwa huko Shanghai leo Jumatano, wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema, kisha atasafiri kwenda mji mkuu wa Korea Kusini, Seoul.

Viongozi wa dunia kukutana wiki ijayo

Ziara hii inakuja kabla ya mkutano kuhusu Tabianchi utakaofanyika wiki ijayo na watashiriki mkutano huo Rais wa Marekani Joe Biden na viongozi wa nchi mbalimbali duniani.

Wizara ya mambo ya nje imesema John Kerry "atajadili juu ya marekebisho ya matarajio ya Tabianchi duniani."

Mkutano wa kwanza wa ngazi ya juu wa mawaziri kati ya Washington na Beijing mwezi uliopita ulizua mabishano na kusababisha mvutano mkubwa kati ya mataifa haya mawili makubwa ya kiuchumi duniani, chini ya miezi miwili baada ya Joe Biden kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi.