MAREKANI

Marekani kuwawekea vikwazo vipya maafisa wa Urusi

Rais wa Urusi Vladimir Putin, Novemba 20, 2020..
Rais wa Urusi Vladimir Putin, Novemba 20, 2020.. © Alexei Nikolsky/AP

Utawala wa Biden unapanga kutangaza vikwazo dhidi ya maafisa wa Urusi leo Alhamisi, ambavyo vitawalenga watu na mashirika kadhaa, kulingana na watu kadhaa wanaofahamu suala hilo wakinukuliwa na shirika la habari la REUTERS.

Matangazo ya kibiashara

Vikwazo vinavyolenga maafisa kadhaa wa Urusi vitaambatana na maagizo ya kufurushwa dhidi ya baadhi yao, kulingana na moja ya vyanzo.

Vikwazo hivyo vinasemekana kuwa sehemu ya majibu ya serikali ya Marekani kwa ukiukaji wa usalama wa kimtandao, kitendo kilichotambuliwa mnamo mwezi Desemba ambapo serikali ya Marekani imeihusisha Urusi, na kuathiri programu iliyofanywa na SolarWinds, na kuwapa wadukuzi nafasi ya kudukuwa siri na nyaraka za maelfu ya makampuni na ofisi za serikali ambazo zinatumia bidhaa zake.

Karibu makampuni 30 yanatarajiwa kukabiliwa na vikwazo kwa kukiuka mkataba wa SolarWinds au kuingilia kati katika uchaguzi wa Marekani, na maafisa kadhaa wa Urusi wanapaswa kufukuzwa.

"Uhasama na kutotabirika kwa hatua za Marekani kwa ujumla hutulazimisha kujiandaa kwa hali mbaya zaidi," msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov aliwaambia waandishi wa habari wiki iliyopita.