URUSI

Moscow yajibu vikwazo vya Marekani kwa kuchukua hatua kadhaa

Waziri wa wa mambo ya njee wa Urusi Sergey Lavrov ametangaza, pamoja na mambo mengine, kufukuzwa kwa karibu kwa wanadiplomasia kumi wa Marekani.
Waziri wa wa mambo ya njee wa Urusi Sergey Lavrov ametangaza, pamoja na mambo mengine, kufukuzwa kwa karibu kwa wanadiplomasia kumi wa Marekani. REUTERS/Sergei Karpukhin

Urusi imeijubu Marekani baada ya kuiwekea vikwazo kwa kuwafukuza wanadilpmasia wake na kupiga marufuku maafisa waandamisi wa Marekani kuingi nchini Urusi.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Urusi imebaini kwamba iko tayari kwa wazo la mkutano kati ya Vladimir Putin na Joe Biden, pendekezo "nzuri".

Hatua hii mpya ya Urusi inakuja wakati uhusiano kati ya nchi hizi mbili umeendelea kuzorota kwa madai ya Washington kuishtumu Urusi kuingilia katika uchaguzi wa urais wa Marekani wa mwaka 2020, ujasusi na mashambulio ya kimtandao.

Siku ya Alhamisi Washington ilitangaza vikwazo zaidi vinavyolenga Urusi, ambavyo ni pamoja na kufukuzwa kwa wanadiplomasia kumi wa Urusi na marufuku kwa benki za Marekani kufanya kazi na kampuni au benki yoyote ya Urusi baada ya Juni 14.