URUSI

Urusi yaongeza kikosi chake cha majini katika Bahari Nyeusi

Urusi imeendelea kuimarisha kikosi chake cha majini kwenye Bahari Nyeusi, hatua inayokosolewa na nchi za Magharibi.
Urusi imeendelea kuimarisha kikosi chake cha majini kwenye Bahari Nyeusi, hatua inayokosolewa na nchi za Magharibi. REUTERS/Maxim Shemetov

Meli mbili za kivita za Urusi zimeelekea Jumamosi katika Bahari Nyeusi, ambapo meli 15 ndogo ziliwasili, wakati nchi hiyo ikiendelea kuimarisha uwepo wake wa majini katika ukanda huo katikati mwa mvutano na nchi za Magharibi na Ukraine.

Matangazo ya kibiashara

Zoezi hili linakuja siku moja baada ya Emmanuel Macron, Angela Merkel na Volodimir Zelenski kuitaka Urusi kuondoa vikosi vya ziada ambavyo imekusanya katika wiki za hivi karibuni kwenye mpaka wake na Ukraine na Crimea.

Rais wa Ufaransa, kansela wa Ujerumani na rais wa Ukraine, ambao walikuwa katika ikulu ya Elysée, walionyesha wasiwasi wao juu ya zoezi hili la jeshi kutoka Urusi, kulingana na ofisi ya kansela wa Ujerumani huko Berlin.

URUSI yawatimu wanadiplomasia wa Marekani

Mahusiano pia yamekuwa mabaya kati ya Urusi na Marekani, ambayo inaishutumu Moscow hasa kwa tabia yake ya uhasama dhidi ya Ukraine.

Katika muktadha huu, siku ya Ijumaa Urusi ilitangaza kuwatimua wanadiplomasia 10 wa Marekani kulipiza kisasi hatua ya Washington ya kuwatimua wanadiplomasia 10 wa Urusi.