INDIA

Coronavirus: Boris Johnson afuta ziara yake nchini India

Maafisa mjini New Delhi, India wamesema mji huo utawekwa chini ya vizuizi vikali vya kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona kwa muda wa wiki moja kuanzia usiku wa leo.
Maafisa mjini New Delhi, India wamesema mji huo utawekwa chini ya vizuizi vikali vya kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona kwa muda wa wiki moja kuanzia usiku wa leo. AFP - NARINDER NANU

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amemechukua uamuzi wa kufuta ziara yake aliyokywa amepanga kufanya wiki ijayo nchini Inofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza imetangaza leo Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya serikali ya Delhi wametangza marufuku ya raia kutotembea kwa kupindi cha siku sita kuanzia Jumatatu jioni nchini India, uamuzi uliothibitishwa na mlipuko wa visa vya maambukizi ya virusi vya Corona na kushindwa kwa mfumo wa afya kukabiliana na hali hiyo.

Vitanda hospitalini vimejaa na kuna uhaba wa gesi ya oksijeni.Katika muda wa saa 24 zilizopita, India ambayo ina jumla ya watu bilioni 1.3 imerekodi maambukizi mapya 273,810.

Hiyo ikiwa ni siku ya tano mfululizo ambapo nchi hiyo, imerekodi zaidi ya maambukizi 200,000 kila siku.Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, Waziri wa Afya Arvind Kejiriwal amesema mfumo wa afya wa mji wa New Delhi uko katika hali tete kuhusiana na janga la COVID-19.