URUSI

Urusi: Alexei Navalny aanza kupewa matibabu

Alexei Navalny wakati wa kesi yake huko Moscow mFebruari 20, 2021.
Alexei Navalny wakati wa kesi yake huko Moscow mFebruari 20, 2021. AP - Alexander Zemlianichenko

Baada ya shinikizo kutoka Marekani na Umoja wa Ulaya, mamlaka ya Urusi hatimaye imekubali kushughulikia hali ya afya ya Alexeï Navalny, mkosoaji mkubwa wa rais Vladimir Putin.  Alexeï Navalny amehpelekwa hospitalini kufuatia hatua yake ya kuanzisha mgomo wa kula ambao uumeingia wiki ya tatu.

Matangazo ya kibiashara

Habari hiyoimetolewa leo Jumatatu asubuhi kama taarifa fupi kutoka kwa mamlaka ya Urusi: "Imeamuliwa kwamba Alexeï Navalny anapaswa kupelekwa hospitali ya gereza iliyoko mkoa wa Vladimir".

Alexeï Navalny anapaswa kuhamishiwa katika jela la IK3, lililoko karibu kilomita 80 kutoka eneo ambapo amekua anazuiliwa. Jela hili kubwa la serikali lina vifaa vya matibabu. Mamlaka ya magereza nchini Urusi pia yanadai kuwa hali ya afya ya Alexeï Navalny ni "ya kuridhisha" na kwamba ameandikiwa vitamini, kwa idhini yake.

Alexei Navalny amekuwa kwenye mgomo wa kula tangu mwishoni mwa mwezi Machi, na kulingana na wale walio karibu naye, afya yake imedhoofika sana katika siku za hivi karibuni. Madaktari kadhaa walio karibu na mpinzani huyo wanasema yuko katika hatari ya kifo, kiwango chake cha potasiamu katika damu kinaweza kusababisha anapatwa na maradhi ya moyo. Madaktari hawa walmeomba kwamba Alexey Navalny awekwe mara moja katika chumba cha wagonjwa mahututi.