MAREKANI

Washington yatiwa wasiwasi na hatua ya Urusi kuweka vizuizi kwenye Bahari Nyeusi

Kikosi cha wanamaji cha Urusi kikifanya mazoezi ya kijesi katika Bahari Nyeusi.
Kikosi cha wanamaji cha Urusi kikifanya mazoezi ya kijesi katika Bahari Nyeusi. REUTERS - SERGEY PIVOVAROV

Marekani inasema ina wasiwasi juu ya mpango wa Urusi wa kuzuia meli za kigenikuingia kwenye kwenye baadhi ya sehemu za Bahari Nyeusi, wiozara ya mambo ya nje ya Marekani imesema, ikitoa wito kwa Moscow kusitisha  kupeleka wanajeshi wake kwenye mpaka na Ukraine.

Matangazo ya kibiashara

Mapema Jumatatu, Mkuu wa Sera za Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell alisema Urusi imekusanya zaidi ya wanajeshi 100,000 kwenye mpaka na Ukraine na katika jimbo la Crimea.

Urusi iliimarisha uwepo wake wa majini kwenye Bahari Nyeusi katika siku za hivi karibuni, baada ya kufanya luteka za kijeshi na mazoezi ya kurusha risasi wiki iliyopita, wakati mvutano na Ukraine ukiendelea kutokota.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Ned Price, amelaani mpango wa Urusi wa kuzuia meli za vikosi vya wanamaji za kigeni na vile vile "meli zingine" za nchi za kigeni kukaribia Crimea.