Coronavirus: Zaidi ya vifo vipya 2,000 vyaripotiwa nchini India
Imechapishwa:
India imerekodi visa vipya 295,041 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona kwa siku moja, takwimu rasmi zimeonyesha leo Jumatano, ikiwa ni rekodi tangu kuzuka kwa janga hilo ambalo limefanya idadi ya maambukizi kufuikia hadi milioni 15.6.
Wizara ya Afya pia imeripoti vifo vipya 2,023 vilivyotoka na COVID-19, ikiwa pia ni rekodi ya kila siku tangu kuzuka kwa mgogoro huu wa kiafya, na kufanya idadi ya vifo kufikia 182,553.
Virusi vya Corona (Cov) ni familia ya virusi vinavyosababisha ugonjwa kuanzia mafua ya kawaida hadi magonjwa makali zaidi kama vile matatizo ya kupumua (MERS-CoV) na SARS-CoV.
Virusi vya Corona vya COVID-19 ni mripuko mpya uliogunduliwa mwaka 2019 na havikuwahi kubainika hapo kabla miongoni mwa bindamu. Dalili zake ni pamoja na homa, kikohozi, shida katika kupumua, na katika hali ngumu zaidi, maambukizi yanaweza kusababisha, nimonia, kukosa pumzi, kushindwa kufanyakazi kwa figo na hata kifo.