INDIA

Coronavirus: Visa vipya vyaendelea kuripotiwa India, hospitali zazidiwa

Siku ya Jumatano, wagonjwa 22 wa COVID-19 walifariki dunia katika hospitali ya umma katika jimbo la Maharashtra (magharibi )baada ya mtungi wa oksijeni kuvuja.
Siku ya Jumatano, wagonjwa 22 wa COVID-19 walifariki dunia katika hospitali ya umma katika jimbo la Maharashtra (magharibi )baada ya mtungi wa oksijeni kuvuja. REUTERS - ADNAN ABIDI

India imerekodi visa vipya 332,730 vya maambukizi ya virusi vya Corona katika muda wa saa 24 zilizopita, idadi kubwa zaidi ya visa vya kila siku duniani kwa siku ya pili mfululizo, wakati visa vikiongezeka katika hospitali zilizojaa wagonjwa.

Matangazo ya kibiashara

Idadi ya vifo vipya kutokana na COVID-19 pia imefikia rekodi katika muda wa saa 24 zilizopita ambapo wagonjwa 2,263 wameripotiwa kufariki dunia, wizara ya afya imesema.

Mamlaka kaskazini na magharibi mwa India, hasa katika mji mkuu wa New Delhi, zimzsema hospitali zimejaa na hazina vifaa vya oksijeni.

Moto umewaua watu 13 katika hospitali moja katika viunga vya mji wa Mumbai ambapo wagonjwa wa COVID-19 walikuwa wakitibiwa.

Siku ya Jumatano, wagonjwa 22 wa COVID-19 walifariki dunia katika hospitali ya umma katika jimbo la Maharashtra (magharibi) baada ya mtungi wa oksijeni kuvuja.

Siku ya Alhamisi, India ilikuwa imeripoti visa 314,835 vya maambukizi katika muda wa saa 24 zilizopita, takwimu ambayo tayari iko juu kuliko rekodi ya kila siku ya kesi 297,430 zilizorekodiwa mwezi wa Januari nchini Marekani.