URUSI

Wanajeshi wa Urusi waanza kuondoka wenye mpaka na Ukraine

Baada ya kutazama luteka hizo, waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu alitangaza kumalizika kwa mazoezi na kuliamuru jeshi kuwaondoa wanajeshi waliokuwa wanashiriki mazoezi Crimea na magharibi mwa Urusi na kuwaresha kwenye kambi zao za kudumu.
Baada ya kutazama luteka hizo, waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu alitangaza kumalizika kwa mazoezi na kuliamuru jeshi kuwaondoa wanajeshi waliokuwa wanashiriki mazoezi Crimea na magharibi mwa Urusi na kuwaresha kwenye kambi zao za kudumu. REUTERS - STRINGER

Urusi imeanza kuondoa wanajeshi wake katika maeneo ya mpakani mwa Ukraine ambapo wanajeshi wake walikuwa wameksanywa kwa wiki kadhaa, na kusababisha kuzuka tena kwa mivutano ya kimataifa, Wizara ya Ulinzi imetangaza leo Ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

Alhamisi wiki hii Waziri wa ulinzi wa Urusi aliyaamuru majeshi ya nchi hiyo kurudi kwenye kambi zao za kudumu, kufuatia luteka kubwa katika rasi ya Crimea, ambazo zilihusisha meli za kijeshi, mamia ya ndege za kivita na maelfu ya wanajeshi, katika uoneshaji wa nguvu katikati mwa mzozo na taifa jirani la Ukraine.

Makumi ya maelfu ya wanajeshi watalazimika kurudi kwenye vituo vyao katika siku zijazo.

Ukraine iliishutumu Urusi kwa kupanga mashambulio makubwa ya kijeshi, na kuongeza wasiwasi kati ya washirika wake wa Magharibi. Kwa upande wake, Urusi imekuwa ikisema kila wakati kuwa ni mazoezi ya kawaida ya kijeshi ambayo imekuwa ikifanya.