ARMENIA

Joe Biden atambua mauaji ya kimbari ya Armenia, Uturuki yapinga

Padri Sarkis Petoyan kutoka kanisa la Mtakatifu Gregory na waumini kadhaa wanakusanyika kwa kuadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1915, ambayo rais wa Marekani Joe Biden, ametambua Montebello, California, Marekani.
Padri Sarkis Petoyan kutoka kanisa la Mtakatifu Gregory na waumini kadhaa wanakusanyika kwa kuadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1915, ambayo rais wa Marekani Joe Biden, ametambua Montebello, California, Marekani. REUTERS - DAVID SWANSON

Rais wa Marekani Joe Biden amesema kwamba mauaji ya Waarmenia katika Dola la Ottoman mnamo mwaka1915 ni mauaji ya kimbari, taarifa ya kihistoria ambayo imekosolewa vikali mara moja na Uturuki.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu wa mfano, unavunja miongo kadhaa ya taarifa za tahadhari kutoka Ikulu ya White juu ya sula hili. Uamuzi huu unakujaa wakati kunaripotiwa mvutano kati ya Marekani na Uturuki, nchi mbili ambazo ni wanachama Jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi, NATO.

Uturuki "inafutilia mbali kabisa" uamuzi huu wa rais wa Marekani, ametangaza Waziri wa Mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu, dakika chache baada ya taarifa ya Joe Biden.

"Hatuna la kujifunza kutoka kwa mtu yeyote juu ya maisha yetu ya zamani. Ufanisi wa kisiasa ni usaliti mkubwa wa amani na haki," Mevlut Cavusoglu ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter. "Tunakataa kabisa taarifa hii yenye lengo la kuzua uhasama."

Mamlaka ya Armenia, hata hivyo, imekaribisha uamuzi huo mara moja, ikikibaini kwamba ni uamuzi muhimu hasa katika muktadha wa mvutano wa sasa wa kikanda.