IRAN

Zarif aomba "radhi" kwa familia ya Soleimani baada ya kuvuja kwa matamshi yake

Waziri wa Mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Baghdad, Iraq, Jumatatu Aprili 26, 2021.
Waziri wa Mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Baghdad, Iraq, Jumatatu Aprili 26, 2021. AP - Khalid Mohammed

Wiki moja baada ya kuchapishwa kwa mahojiano ya siri ambayo waziri wa mambo ya nje alionekana kukosoa jukumu la Jenerali Qassem Soleimani, aliyeuawa katika shambulio la Marekani mwezi Januari 2020 huko Baghdad, Mohammad Javad Zarif ameomba "msamaha" kwa familia ya Soleimani kwa matamshi yake.

Matangazo ya kibiashara

Kutokana na kuibuka kwa sintofahamu iliyosababishwa na matamshi ya waziri wa mambo ya nje wa Iran kukosoa jukumu la mkuu wa zamani wa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Iran Quds Jenerali Qassem Soleimani, Mohammad Javad Zarif, hatimaye ameomba "msamaha".

Rekodi ya sauti yake iliyovuja ilisababisha ukosoaji mkubwa nchini Iran dhidi ya waziri wa mambo ya nje kwa kuhoji sera ya mambo ya nje ya mamlaka ya Iran.

"Natumai familia inayoheshimiwa ya Jenerali Qassem Soleimani itanisamehe," waziri huyo ameandika ujumbe huo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Tangu kuchapishwa kwa rekodi hii na vyombo vya habari vya Iran vilio nje ya nchi, wahafidhina wameendelea kumkosoa waziri wa mambo ya nje.