INDIA

Coronavirus: Idadi ya vifo nchini India yakaribia Milioni 20

Nchi mbalimbali zaendelea kutuma misaada ya kimatibabu India.
Nchi mbalimbali zaendelea kutuma misaada ya kimatibabu India. REUTERS - RUPAK DE CHOWDHURI

India imerekodi zaidi ya visa vipya 300,000 vya maambukizi ya virus vya Corona katika muda wa saa ishirini na nne kwa siku ya kumi na mbili mfululizo, na kufanya idadkuzuka kwa janga hilo nchini humo, kulingana na takwimu rasmi zilizotolewa leo Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Takwimu kutoka Wizara ya Afya pia zinaonyesha vifo vipya 3,417 kutokana na COVID-19 kwa siku moja, kwa jumla ya vifo 218,959 tangu kuzuka kwa mgogoro  huo wa kiafya nchini India.

Kulingana na baadhi ya wataalam wa matibabu, idadi halisi ya visa vya maambukizi naweza kuwa juu mara kumi kuliko idadi rasmi.

Wakati hospitali zinakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na uhaba oksijeni, majimbo na wilaya kadhaa nchini zimeweka vizuizi vya kiafya kwa matumaini ya kudhibiti janga hili baya.

Serikali ya Waziri Mkuu Narendra Modi hata hivyo inasita kutoa uamuzi wa kitaifa, kwa kuhofia athari za kiuchumi za hatua hiyo.

Huu ni mgogoro mbaya zaidi ambao Narendra Modi amekumbana nao tangu aingie madarakani mwaka 2014. Kiongozi huyo wa India amekosolewa kwa kukosa kuchukua hatua dhidi ya mgogoro huu wa kiafya mapema.