INDIA-AFYA

COVID-19: Virusi vyasambaa haraka kusini mwa India

Bangalore imekuwa jiji lililoathirika zaidi nchini India. Siku ya Jumatano, iliripoti visa 23,000 katika muda wa saa 24, sawa na 10% zaidi ya New Delhi.
Bangalore imekuwa jiji lililoathirika zaidi nchini India. Siku ya Jumatano, iliripoti visa 23,000 katika muda wa saa 24, sawa na 10% zaidi ya New Delhi. AFP - MANJUNATH KIRAN

India imevunja rekodi mpya ya dunia ya maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 siku ya Jumatano baada ya visa 412,000 kuripotiwa kwa muda wa saa 24 kwa vifo 3,600, wakati idadi ya watu wanaofanya vipimo imepungua sana katika siku za hivi karibuni

Matangazo ya kibiashara

Miji mikubwa iliyoathiriwa kwanza, kama New Delhi na Mumbai, imeanza kuona maambukizi yakipungua , lakini virusi hivi sasa vinasambaa haraka sana kusini mwa nchi.

Tukio hilo lilitokea Jumatano asubuhi katika hospitali ya umma nje kidogo ya Madras, kusini mwa India: wagonjwa 447 wanatibiwa na 70% ya hao wanahitaji msaada wa kupumua. Wakati shinikizo la oksijeni likipunguwa ghafla: Wagonjwa tisa hufariki dunia ndani ya muda wa masaa kadhaa kwa kukosa hewa. Wengine wawili walifariki dunia kwa sababu hiyo hiyo wakati wa mchana.

Matumizi ya oksijeni yaliongezeka maradufu kwa wiki moja, umesema uongozi wa hospitali hii ya umma, kwa sababu ya kuwasili kwa wagonjwa wa COVID-19.

Tukio hilo lilikuwa likitokea kaskazini mwa India na hasa katika eneo la New Delhi hadi sasa. Mgogoro wa kiafya sasa unayakumba maeneoya kusini mwa nchi.

Kwa mfano, Bangalore imekuwa jiji lililoathirika zaidi nchini India. Siku ya Jumatano, iliripoti visa 23,000 katika muda wa saa 24, sawa na 10% zaidi ya New Delhi.