AUSTRALIA

Australia: Mipaka kutofunguliwa kikamilifu hadi katikati ya mwaka wa 2022

Watu hawa, ambapo baadhi wamevaa barakoa, wakisubiri kusafiri kwenye kituo kikuu cha treni, baada ya kutangazwa hatua mpya zinazohusiana na afya katikakukabiliana na janga la COVID-19.
Watu hawa, ambapo baadhi wamevaa barakoa, wakisubiri kusafiri kwenye kituo kikuu cha treni, baada ya kutangazwa hatua mpya zinazohusiana na afya katikakukabiliana na janga la COVID-19. REUTERS - LOREN ELLIOTT

Australia inasema kuna uwezekano wa kufungua tena mipaka yake ya kimataifa kabla ya katikati ya mwaka 2022, Waziri wa Biashara wa Australia Dan Tehan amesema leo Ijumaa, na kukatisha tamaa kwa mashirika ya ndege na sekta ya utalii.

Matangazo ya kibiashara

Alipoulizwa ni lini mipaka itafunguliwa wakati wa mahojiano na kituo cha Sky News, Dan Tehan amejibu kwamba "nadhani bora iwe katikati ya mwaka ujao, lakini kama tulivyoona katika janga hili, mambo yanaweza kubadilika."

Waziri huyo ameongezea kwamba ana imani kwamba kuna mfumo mwingine wa kusafiri ambao unaweza kufunguliwa, kama ule uliyopo kati ya Australia na New Zealand.