JAPAN-AFYA

Serikali ya Japan yataka kuongeza hali ya dharura hadi Mei 31

Katika ngazi ya kitaifa, Japani imerekodi visa 618,197 vya maambukizi ya aina mpya ya kirusi cha Corona na karibu vifo 10,585 kutokana na COVID-19 vimethibitishwa, kulingana na takwimu za serikali.
Katika ngazi ya kitaifa, Japani imerekodi visa 618,197 vya maambukizi ya aina mpya ya kirusi cha Corona na karibu vifo 10,585 kutokana na COVID-19 vimethibitishwa, kulingana na takwimu za serikali. AP - Eugene Hoshiko

Serikali ya Japan inapanga kuongeza muda wa hali ya tahadhari katika mji mkuu wa nchi  hiyo Tokyo na mikoa mingine mitatu kwa wiki tatu, hadi mwisho wa mwezi Mei, ili kuzuia kuongezeka kwa visa vipya vya Corona miezi michache kabla ya kuanza kwa Michezo ya Olimpiki ya Tokyo, waziri wa afya amesema leo Ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

Serikali ilikuwa na matumaini kuwa hali ya dharura "fupi na yenye nguvu" ingewezesha kudhibii mlipuko wa nne wa maambukizi, lakini kesi mpya katika mji mkuu Tokyo na mji wa pili kwa ukubwa Osaka bado ziko katika viwango vya juu, waziri huyo mwenye dhamana inayohusiana na janga hilo amesema.

Kuongeza muda wa hali ya tahadhari kutoka Mei 11 hadi Mei 31 itatoa nafasi kwa kipindi cha miezi miwili kabla ya kuanza kwa michezo ya Olimpiki Julai 23, ambayo tayari imeahirishwa kwa mwaka kwa sababu ya janga hilo.

"Mji wa Osaka hasa uko katika hali hatari kwa mfumo wake wa matibabu," Yasutoshi Nishimura amesema mwanzoni mwa mkutano na jopo la wataalam wa matibabu na uchumi, akibainisha kuwa aina tofauti zinaenea haraka.

Katika ngazi ya kitaifa, Japani imerekodi visa 618,197 vya maambukizi ya aina mpya ya kirusi cha Corona na karibu vifo 10,585 kutokana na COVID-19 vimethibitishwa, kulingana na takwimu za serikali.