INDIA-AFYA

India: Miili ya watu wanaodhaniwa kufariki kwa Corona yaelea kwenye Mto Ganges

India inaendelea kukabiliwa na ongezeko la maabukizi na vifo vingi kutokana na Corona.
India inaendelea kukabiliwa na ongezeko la maabukizi na vifo vingi kutokana na Corona. REUTERS - DANISH SIDDIQUI

Picha za kutisha za miili iliyojazana kwenye kingo za Mto Ganges zinasambaa kote India. India inaendelea kushuhudia visa vingi vya maambukizi na fifo kutokana na janga hilo hatari.

Matangazo ya kibiashara

Picha hizi zilipigwa katika kambi ya Chausa, ambayo ni sehemu ya wilaya ya Buxar, katika jimbo la mashariki la Bihar.

Serikali ya eneo hilo ilithibitisha tukio hilo Mei 10, lakini ikasema miili hiyo inaweza kuwa ilielea kutoka mji jirani wa Uttar Pradesh. "Karibu miili 30 hadi 40 imepatikana kwene Mto Ganges," amesema Ashok Kumar, afisa wa eneo hilo.

"Inawezekana kwamba miili hiyo ilishuka mtoni kutoka mji wa Uttar Pradesh. Nimezungumza na wakazi kdhaa ambao wanasema miili hiyo haikutokea katika eneo hilo."