HONG KONG

Hong Kong yazuia mali za Jimmy Lai

Tajiri mmiliki wa vyombo vya habari huko Hong Kong, Jimmy Lai mwenye umri wa miaka 73 alihukumiwa kifungo cha miezi 12 jela.
Tajiri mmiliki wa vyombo vya habari huko Hong Kong, Jimmy Lai mwenye umri wa miaka 73 alihukumiwa kifungo cha miezi 12 jela. Anthony WALLACE AFP/File

Mamlaka Hong Kong imechukua uamuzi wa kuzuia mali za mmiliki wa vyombo vya habari Jimmy Lai, ambaye mwezi uliopita alihukumiwa kifungo cha miezi 14 jela kwa kushiriki katika maandamano ya kupinga demokrasia katika kanda Maalum ya Utawala ya China mwaka 2019.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa mali zilizozuiliwa ni pamoja na hisa za Jimmy Lai katika ampuni ya Next Digital Limited na pia hisa zake katika akaunti za benki ya Hong Kong za kampuni tatu anazomiliki.

Jimmy Lai amekuwa kizuizini tangu mwezi Desemba kwa sababu ya mashtaka chini ya mfumo wa sheria mpya ya usalama wa kitaifa iliyowekwa mwezi Juni 2020 huko Hong Kong kwa mpango wa serikali ya Beijing.