CHINA-MAREKANI

China yadai kuwa Marekani inatishia amani katika Mlango wa Taiwan

Bendera za China na Marekani zinapepea nje ya jengo la kampuni huko Shanghai, China Aprili 14, 2021.
Bendera za China na Marekani zinapepea nje ya jengo la kampuni huko Shanghai, China Aprili 14, 2021. © REUTERS/Aly Song/File Photo

China imeishutumu Marekani kwa kutishia amani na utulivu wa Mlango wa Taiwan baada ya meli ya kivita ya Marekani kuvuka ukingo huo.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema meli kubwa ya kijeshi, USS Curtis Wilbur, ilivuka ukingo Mlango wa Taiwan kwa kazi yao ya kila siku Jumanne, kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

"Kupita kwa meli kupitia Mlango wa Taiwan kunaonyesha nia ya Marekani kwa eneo huru na la wazi la Indo-Pacific. Jeshi la Marekani litaendelea kurusha ndege zake, kutumia meli zake na kufanya kazi popote pale sheria ya kimataifa inaruhusu."

Msemaji wa Jeshi la Ukombozi la Watu wa China ameelezea upinzani wake mkali na kulaani hatua hiyo, ambayo inakuja wakati wa mvutano mkubwa kati ya serikali hizo mbili.

Mvutano wa kijeshi kati ya Taiwan na Beijing umeongezeka zaidi ya mwaka uliopita, huku Taipei ikilalamika kuwa China inapeleka vikosi vyake vya anga mara kwa mara katika eneo la ulinzi wa anga la Taiwan.

China imesema shughuli zake karibu na Taiwan zinalenga kulinda uhuru wa China. Serikali ya Taiwan imeishutumu kama inajaribu kufanya vitisho.