TAIWAN-AFYA

Taiwan kupokea dozi 400,000 za chanjo za COVID-19

Karibu dozi 400,000 zaidi zitawasili Taiwan Jumatano alasiri kutoka Amsterdam, msemaji wa serikali Lo Ping-cheng ameiwaambia waandishi wa habari.
Karibu dozi 400,000 zaidi zitawasili Taiwan Jumatano alasiri kutoka Amsterdam, msemaji wa serikali Lo Ping-cheng ameiwaambia waandishi wa habari. REUTERS - ANN WANG

Taiwan itapokea dozi zingine mpya 400,000 za chanjo ya AstraZeneca dhidi ya COVID-19 leo Jumatano kama sehemu ya mpango wa ugawanai chanjo ya COVAX, serikali imesema, wakati nchi hii inakabiliwa na upungufu wa chanjo na ongezeko la maambukizi.

Matangazo ya kibiashara

Taiwan imeripoti karibu visa vipya 1,000 vya maambukizi katika wiki iliyopita, na kusababisha malmaka kuweka masharti mapya katika mji mkuu Taipei na wakati janga hilo lilikuwa chini ya udhibiti.

Chanjo iliyopo nchini inaisha haraka. Kufikia sasa, Taiwan imepokea tu dozi karibu 300,000, zote za AstraZeneca na angalau theluthi mbili ya chanjo hizi zimetolewa.

Karibu dozi 400,000 zaidi zitawasili Taiwan leo Jumatano alasiri kutoka Amsterdam, msemaji wa serikali Lo Ping-cheng ameiwaambia waandishi wa habari.

Taiwan inatarajia kupokea dozi zaidi ya milioni moja ya AstraZeneca kupitia mpango wa COVAX.