BURMA

Burma: Mamlaka ya kijeshi kufuta chama cha Aung San Suu Kyi

Mamlaka ya kijeshi, ambayo ilichukua madaraka Februari 1 na ambayo inaendelea kumzuia Aung San Suu Kyi, inasema ushindi mkubwa wa chama cha NLD katika uchaguzi wa Novemba ulitokana na udanganyifu.
Mamlaka ya kijeshi, ambayo ilichukua madaraka Februari 1 na ambayo inaendelea kumzuia Aung San Suu Kyi, inasema ushindi mkubwa wa chama cha NLD katika uchaguzi wa Novemba ulitokana na udanganyifu. REUTERS - POOL

Tume ya uchaguzi iliyoteuliwa na mamlaka ya kijeshi nchini Burma itafuta chama LND cha Aung San Suu Kyi, wakimtuhumu kwa udanganyifu mkubwa katika uchaguzi wa wabunge mwezi Novemba mwaka uliyopita, shirika la habari la Myanmar Now limeripoti, likimnukuu mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo umechukuliwa wakati wa mkutano na vyama vya siasa, mkutano ambao umesusiwa na vyama vingi, ikiwa ni pamoja na chama cha NLD, shirika la habari la Myanmar Now limeongeza.

Mamlaka ya kijeshi, ambayo ilichukua madaraka Februari 1 na ambayo inaendelea kumzuia Aung San Suu Kyi, inasema ushindi mkubwa wa chama cha NLD katika uchaguzi wa Novemba ulitokana na udanganyifu, ingawa wakati huo tume ya uchaguzi ilikataa mashtaka haya.

Udanganyifu huu wa uchaguzi ulikuwa kinyume cha sheria "na kwa hivyo tutalazimika kufuta chama ca NLD," amesema Thein Soe, mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (UEC),  akinukuliwa na shirika la habari la Myanmar Now.

Thein Soe ameongeza kuwa wale waliofanya udanganyifu huo watachukuliwa kuwa "wasaliti" na kwamba hatua zitachukuliwa dhidi yao.