KOREA KUSINI-MAREKANI

Marekani: Rais wa Korea Kusini kuwa kiongozi wa pili kupokelewa na Joe Biden

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in azungumza wakati wa mkutano na Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi katika makao maku ya Bunge, Capitol Hill, huko Washington, Marekani, Mei 20, 2021.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in azungumza wakati wa mkutano na Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi katika makao maku ya Bunge, Capitol Hill, huko Washington, Marekani, Mei 20, 2021. REUTERS - POOL

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in atakuwa kiongozi wa pili duniani kupokelewa na Rais wa Marekani Joe Biden katika Ikulu ya White Ijumaa hii, na wa pili kutoka bara la Asia, ishara muhimu ambayo Washington inaonyesha kwa ukanda huo katika juhudi zake za kupinga ushawishi wa China .

Matangazo ya kibiashara

Mbali na suala la kudumu la mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini, wawili hao watajadili usalama kwa mapana zaidi usalama wa kikanda, ushirikiano katika tasnia ya teknolojia ya hali ya juu kama microprocessors, juhudi za kudhibiti janga la Corona, na njia za kuimarisha hatua dhidi ya Tabia nchi.

Moon Jae-in anatarajia kupata makubaliano na Washington kwa usambazaji wa chanjo ya COVID-19, wakati utawala wa Biden unatarajia ahadi kali za Tabia nchi kutoka Seoul.

Washington pia inatarajia kuona kauli ya ukweli ya Moon Jae-in juu ya tabia ya China inayozidi kuwa na nguvu katika ukanda huo. Mwezi uliopita, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Japani Yoshihide Suga, Joe Biden alitaka kuwepo na umoja dhidi ya Beijing.

Viongozi hao wawili watakutana na kisha kufanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari saa 11 jioni kwa saa za Marekani.