TAIWAN-AFYA

Taiwan yaishutumu China kwa kutumia chanjo kwa malengo ya kisiasa

Wafanyakazi wa matibabu huandaa chanjo ya COVID-19 katika Hospitali ya Far Eastern Memorial huko New Taipei City, Machi 22, 2021.
Wafanyakazi wa matibabu huandaa chanjo ya COVID-19 katika Hospitali ya Far Eastern Memorial huko New Taipei City, Machi 22, 2021. AFP - SAM YEH

Taiwan, kisiwa chenye wakaazi milioni 24 kinachodaiwa na Beijing kuwa ni sehemu yake ya bardhi, kimekuwa kikikabiliwa kwa siku kadhaa na kuibuka tena kwa janga la Corona (zaidi ya kesi elfu moja kwa wiki) ambalo linadhoofisha mkakati wake wa "kudhibiti COVID-19".

Matangazo ya kibiashara

Katika muktadha wa uhaba wa dozi za chanjo, serikali iimebaini kwamba Beijing inatumia chanjo hiyo kutekeleza ajenda zake za kisiasa.

"Wataiwan hawana imani ya kutosha na chanjo kutoka China," amesema naibu mkurugenzi wa kituo cha kuzuia na kudhibiti janga la Corona huko Taiwan leo Jumamosi. Kutokana na kuibuka tena kwa janga huko Taiwan tangu mwa wiki iliyopita, msaada wa China kwa Taiwan umetoa ulikosolewa katika siku za hivi karibuni ili kushawishi serikali kukubali utumiaji wa chanjo kutoka China, ingawa imepigwa marufuku kwenye ardhi ya Taiwan.

Asilimia 1 ya wakazi wa Taiwan ndio pekee wamepewa chanjo dhidi ya Corona. Taipei, ambayo ilikuwa inategemea hasa chanjo yake iliyozalishwa katika kisiwa hicho - inayotarajiwa kwa msimu wa joto - ili kumaliza kampeni yake ya chanjo, ilikuwa imepokea wiki iliyopita dozi 300,000 kati ya dozi milioni 20 zilizoagizwa kutoka kwa maabara ya Moderna na AstraZeneca.