INDIA-

Coronavirus / India: Idadi ya visa vya maambukizi yapindikia Milioni 27

Jumla ya visa nchini India sasa vimefikia Milioni 27.16, wakati idadi ya vifo vyote vikifika 311,388, kulingana na takwimu zilizotolewa na wizara ya afya.
Jumla ya visa nchini India sasa vimefikia Milioni 27.16, wakati idadi ya vifo vyote vikifika 311,388, kulingana na takwimu zilizotolewa na wizara ya afya. © REUTERS - ADNAN ABIDI

Idadi ya maambukizi ya Corona nchini India imezidi Milioni 27 leo Jumatano, na visa vipya 208,921 vimerekodiwa katika muda wa saa 24 zilizopita, wakati idadi ya vifo vya kila siku kutokana na COVID-19 ikiongezeka hadi 4,157.

Matangazo ya kibiashara

Jumla ya visa nchini India sasa vimefikia Milioni 27.16, wakati idadi ya vifo vyote vikifika 311,388, kulingana na takwimu zilizotolewa na wizara ya afya.

Hayo yanajiri wakati viongozi wa Umoja wa Ulaya wameafiki kibali cha kidijitali cha COVID-19 kwa wasafiri miongoni mwa mataifa wanachama kama hatua ya kuwezesha usafiri, utalii na kukuza uchumi wakati huu wa msimu wa joto.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya walikubaliana Jumanne hii kuchanga dozi zisizopungua milioni 100 za COVID-19 kwa nchi masikini ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Umoja huo unatarajia kupokea zaidi ya dozi bilioni moja kutoka kwa kampuni nne za kutengeneza chanjo ifikapo mwisho wa mwezi Septemba.