CHINA

China: Ruksa kwa familia kupata watoto watatu

"Kwa kukabiliana na kuzeeka kwa raia (...), wanandoa wanaruhusiwa kupata watoto watatu," shirika la habari la serikali limeripoti shirika la habari la serikali la New China.
"Kwa kukabiliana na kuzeeka kwa raia (...), wanandoa wanaruhusiwa kupata watoto watatu," shirika la habari la serikali limeripoti shirika la habari la serikali la New China. Noel Celis AFP/File

China imeamua kuondoa kikomo cha watoto wawili kwa wanandoa na kuruhusu familia kuwa na watoto hadi watatu, kwa kukabiliana na idadi ya watu waliozeeka, Shirika la habari la taifa la Xinhua limetangaza Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo inakuja wiki chache baada ya kuchapishwa kwa matokeo ya sensa ya mwisho ya miaka kumi, ambayo yalifichua kupungua kwa kasi kwa kiwango cha watoto kuzaliwa katika nchi yenye watu wengi zaidi duniani.

"Kwa kukabiliana na kuzeeka kwa raia (...), wanandoa wanaruhusiwa kupata watoto watatu," shirika la habari la serikali limeripoti, likinukuu hitimisho la mkutano wa ofisi ya kisiasa ya Chama cha Kikomunisti uliyoongozwa na rais Xi Jinping .

Kuzeeka haraka kwa raia

Mwanzoni mwa mwezi Mei, matokeo ya sensa yaliyotolewa mwaka 2020 yalibaini hali ya kuzeeka haraka kuliko ilivyotarajiwa kwa raia wa China. Mwaka jana, mwaka uliokumbwa na janga la ugonjwa wa COVID-19, idadi ya watoto waliozaliwa ilishuka hadi milioni 12, dhidi ya milioni 14.65 mnamo mwaka 2019. Mwaka huo, kiwango cha watoto kuzaliwa (10.48 kwa 1,000) kilikuwa chini kabisa tangu kuanzishwa kwa China ya Kikomunisti mnamo mwaka 1949.

Baada ya zaidi ya miongo mitatu ya "sera ya mtoto mmoja," China ililegeza sheria zake mnamo waka 2016, ikiruhusu raia wote wa China kupata mtoto wa pili. Lakini bila kufanikiwa kuanzisha upya kiwango cha kuzaliwa.

Kuna sababu nyingi za kushuka kwa kiwango cha kuzaliwa: kushuka kwa idadi ya ndoa, kuongezeka kwa gharama kuhusiana na kodi ya ya nyumba na elimu, na kuchelewesha kuzaa kwa wanawake ambao wanatoa kipaumbele zaidi kwa kazi zao.

Zaidi ya watu milioni 264 wenye umri wa miaka 60 na zaidi mwaka 2020

Mwaka jana, China ilikuwa na zaidi ya watu milioni 264 wenye umri wa miaka 60 na zaidi, mara nne ya jumla ya wananchi wa Ufaransa.

Kundi hili la umri sasa ni jumla ya asilimia 18.7, ongezeko la asilimia 5.44 ikilinganishwa na sensa ya mwaka 2010. Kinyume chake, idadi ya watu wenye umri wa kufanya kazi (miaka 15 hadi 59) ni jumla ya 63.35% tu, ilishuka alama 6.79 kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10.

Mnamo Machi, bunge lilipiga kura juu ya mpango wa kuongeza hatua kwa hatua umri wa kustaafu katika kipindi cha miaka mitano ijayo.