UTURUKI-HAKI

Mpwa wa Erdogan atekwa nyara Kenya na wapelelezi wa Uturuki

Rais aw Uturuki Recep Tayyip Erdogan na mhubiri Fethullah Gülen, mpinzani wake mkuu, anayeishi nchini Marekani
Rais aw Uturuki Recep Tayyip Erdogan na mhubiri Fethullah Gülen, mpinzani wake mkuu, anayeishi nchini Marekani AFP PHOTO / THIERRY CHARLIER / ZAMAN DAILY / SELAHATTIN SEVI

Maafisa wa ujasusi wa Uturuki wamemkamata nje ya nchi na kumrudisha nyumbani mpwa wa mhubiri Fethullah Gülen, adui nambari moja wa Rais Recep Tayyip Erdogan, vyombo vya habari vimeripoti Jumatatu, huku mke wa Selahaddin Gülen akisema alikuwa "ametekwa" nchini Kenya.

Matangazo ya kibiashara

Selahaddin Gülen amerudishwa nchini Uturuki na maafisa wa idara ya ujasusi ya nchi hiyo (MIT) baada ya kukamatwa nje ya nchi, shirika la habari la serikali Anadolu limeripoti, bila kutaja nchi ambako alikamtwa.

Kwenye video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii Mei 20, mkewe alidai kwamba wote wawili wanaishi Kenya na kwamba alikuwa hana taarifa yoyote kuhusiana na mumewe tangu Mei 3, wakati mume wake alikuwa akifundisha katika shule moja jijini Nairobi.

"Kiongozi wa kigaidi", kulingana na Erdogan

Watu na vyombo vya habari vyenye uhusiano na chama cha Fethullah Gülen pia wamesema kwenye mitandao ya kijamii kwamba Selahaddin Gülen "alitekwa nyara" nchini Kenya, na wameanzisha kampeni ya kutaka aachiliwe.

Selahaddin Gülen anatuhumiwa na maafisa wa Uturuki kuwa na uhusian na "shirika la kigaidi la Fetö", neno linalotumiwa na serikali ya Ankara kwa kutaja chama cha mhubiri Fethullah Gülen. Recep Tayyip Erdogan, ambaye wakati mmoja alikuwa uhusiano na Selahaddin Gülen, leo anamtaja kama "kiongozi wa kigaidi" na anamshtumu kwa kuwa alifanya jaribio la mapinduzi dhidi yake mwezi Julai 2016.